Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:16

Watu wenye silaha wawateka walimu na wanafunzi Nigeria


Kundi la wasichana waliokuwa wametekwa nyara katika shule ya Bweni iliyoko Kaskazini Magharibi Februari 26, 2022. Picha na Aminu ABUBAKAR / AFP.
Kundi la wasichana waliokuwa wametekwa nyara katika shule ya Bweni iliyoko Kaskazini Magharibi Februari 26, 2022. Picha na Aminu ABUBAKAR / AFP.

Serikali ya Nigeria imesema Jumanne kwamba watu wenye silaha wamewateka nyara wanafunzi sita na walimu watatu kutoka shule moja katika jimbo la Kusini Magharibi la Ekiti usiku wa Jumatatu, hii ikiwa ni ripoti ya kwanza ya utekajinyara inayohusisha wanafunzi kwa mwaka huu.

Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakiwateka wanakijiji, wasafiri wa barabarani na wanafunzi kwa kudai fidia, katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, ambayo inapambana na ukosefu mkubwa wa usalama, pamoja na uwasi wa muda mrefu unaofanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu huko Kaskazini Mashariki.

Serikali ya Ekiti imesema katika taarifa utekaji huo wa hivi karibuni umetokea wakati wanafunzi na walimu walipokuwa wakirudi kutokasafari karibu na kijiji chao siku ya Jumatatu usiku. Dereva wa basi hilo la shule pia alitekwa.

Idara za usalama katika jimbo wako kwenye msako wa kuwatafuta watekaji nyara hao, taarifa hiyo iliongeza.

Hakuna aliyedai kuwajibika au kudai fidia. Rais Bola Tinubu, anaewekea kuufufua uchumi wa nchi hiyo unaosuasua kuwa kipaumbele chake, anazidi kuwekewa shinikizo kutokana na wimbi la utekaji nyara katika nchi nzima ya Nigeria, yakiwemo maeneo yaliyoko nje ya mji mkuu wa Abuja mwezi huu.

Kiongozi mkuu wa upinzani Atiku Abubakar siku ya Jumanne alimshtumu Tinubu kwa “kucheza fidla” wakati Nigeria ikizama baharini kwa kutokuwa na usalama” akijaribu kutaja ziara binafsi ya rais amefanya safari binafsi ya wiki kwenda Ufaransa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG