Mashambulizi kati ya wakulima na wafugaji na mizozo ya kijamii imekithiri katikati mwa Nigeria, eneo lenye makabila na madini tofauti linalojulikana kama the “Middle Belt” ambapo machafuko ya mara kwa mara yalisababisha vifo vya mamia ya watu katika miaka ya hivi karibuni.
Machafuko ya hivi karibuni siku ya Jumatano yametokea baada ya shambulio la siku ya Christmas katika eneo hilo ambalo liliua takriban watu 140. Amri ya kutotoka nje usiku iliwekwa tarehe 23 Januari.
Msemaji wa polisi katika jimbo la Plateau hakujibu mara moja ombi la Reuters kutoa maelezo kuhusu mashambulizi hayo yaliyofanyika kwa siku mbili.
Forum