Taasisi ya Bill & Melinda Gates itatoa dola milioni 40 ikiwemo kampuni ya Biotech ya ubelgiji na nyingine mbili za Afrika zinazoongoza kwa utengenezaji wa chanjo katika harakati za kuinua chanjo za mRNA kuzuiya magonjwa mbalimbali Afrika.
Kampuni ya Quantoom Biosiences yenye makao yake Mivelles itapata dola milioni 20 kuendeleza kazi ya utengenezaji chanjo za mRNA, wakati institut Pasteur de Dakar ya nchini Senegal na ile ya Biovac ya Afrika Kusini zitapata dola milioni 5 kila moja kununua teknolojia hiyo.
Dola milioni 10 zaidi zitatolewa kwa watengenezaji wengine wa chanjo ambao wanataka kutumia jukwaa hilo.
Chanjo zilizo tengenezwa kwa kutumia mRNA zilibadilisha majibu ya ulimwengu katika janga la COVID – 19, lakini ufikiaji haukuwa sawa.
Juhudi kadhaa zimeanzishwa ili kukabiliana na hili na kujaribu kutumia teknolojia mpya kwa vitisho vilivyopo ambavyo vinaathiri vibaya nchi za kipato cha chini kama vile malaria na kifua kikuu.
Shirika la Afya Duniani lilianzisha teknolojia ya chanjo yake ya mRNA huko cape town mwezi April mwaka 2023.