Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia tangazo hilo, Savola alisema kuwa vifaru vinavyotumwa ni vya muundo wa Leopard 2 ulioimarishwa, na vimeundwa mahsusi kwa ajili ya kusafisha maeneo yenye vilipuzi vingine.
"Tutatuma vifaa zaidi vya ulinzi na kushirikiana na washirika wetu," Waziri wa Ulinzi wa Finland Mikko Savola alisema katika taarifa.
Msaada huo pia utajumuisha "mafunzo yanayohusiana na matumizi na matengenezo ya vifari hivyo," kwa mujibu wa waziri huyo.
Kati ya vifaru 200 yva Leopard 2 vinavyomilikiwa na Finland, ni sita pekee vilivyorekebishwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu kama hayo. Finland, ambayo mpaka wake na Russia ni takriban kilomita 1,300, imekuwa ikisita kujitolea kutuma vifaru vya vita nchini Ukraine.
Tangazo hilo linafuatia ahadi ya vifaru sita kutoka Uhispania siku ya Jumatano na linajiri baada ya Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kusema Ijumaa wiki jana, kwamba washirika walio na vifaru vya vita wanapaswa kuvituma sasa.
Hapo awali Ujerumani ilipinga shinikizo kutoka kwa washirika kuidhinisha uwasilishaji wa vifaru vya Leopard, viliyotengenezewa Ujerumani, kutumwa Ukraine.