Vifaru hivyo vilitengenezwa katikati ya miaka ya 60 hadi katikati ya miaka ya 80, lakini havitawafikia wapiganaji wa Kyiv hadi miezi ya msimu wa joto.
Lakini mawaziri wa ulinzi wa Ujerumani, Denmark na Uholanzi wamesema katika taarifa kwamba zana hizo za ziada zitaimarisha vya kutosha uwezo wa kijeshi wa Ukraine ili kuyadhibiti tena maeneo yake yaliyotekwa.
Wizara ya ulinzi ya Ujerumani imesema mamlaka za Berlin zimeidhinisha kusafirisha nchini Ukraine hadi vifaru 178 aina ya Leopard 1 A 5, lakini imesema idadi hiyo itakayopelekwa huko itategemea uboreshaji unaohitajika.
Zana hizo mpya zikazopelekwa ni kufuatia tangazo la hivi karibuni la Ujerumani kwamba itapeleka vifaru 14 vipya aina ya Leopard 2 kwa wapiganaji wa Ukraine.
Marekani ilisema itatoa vifaru vyake 30 aina ya Abrams.