Familia Ethiopia and Sudan zaishitaki Marekani kwa ucheleweshaji wa visa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken

Familia za Wasudan na Waethiopia ambazo zilishinda bahati nasibu ya kuwaruhusu kuhamia Marekani wameishitaki serikali kwa mchakato wa kuchelewesha kupata VISA.

Familia 12 zimewisilisha kesi hiyo, inayofahamika kama Tesfaye vs Blinken, zinasema serikali ya Marekani kinyume cha sheria kimezuia mchakato wa kuwasikiliza kuhusu utoaji wa visa dhidi yao kwa kukataa kuzipeleka kesi hizo katika balozi nyingine mbali na zile za Khartoum na Addis Ababa ambazo hazijaanza tena kushughulikia mchakato wa VISA.

Chini ya sheria ya uhamiaji na utaifa ya Marekani washindi wote wa program ya visa ya wahamiaji wanatakiwa wafanyiwe mahojiano kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha ambao ni septemba 30, isipokuwa kama mahakama itaingilia.

Mmoja wa mawakili wanaowakilisha familia amesema wanayo fursa ya mara moja katika maisha yao kuwa wakazi wa kudumu lakini serikali inaendelea kupunguza umuhimu wa kesi zao.

Wakili mwingine Rafael Urena amesema marekani imeshindwa kutekeleza ahadi zake kwa waafrika , hasa kwa waombaji wa visa hiyo inayojulikana zaidi kama Diversity visa lottery.