Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 17:10

WFP yatahadharisha njaa kali kaskazini mwa Ethiopia


FILE - Wakimbizi waliokimbia vita mkoa wa Tigray na samani na punda wao katika eneo la bonde la mto Tekeze katika mpaka wa Sudan-Ethiopia, huko Hamdayet, mashariki ya Sudan, Nov. 21, 2020.
FILE - Wakimbizi waliokimbia vita mkoa wa Tigray na samani na punda wao katika eneo la bonde la mto Tekeze katika mpaka wa Sudan-Ethiopia, huko Hamdayet, mashariki ya Sudan, Nov. 21, 2020.

Shirika la Chakula Duniani, WFP, linaonya kutokea njaa kali kaskazini mwa Ethiopia.

Mashirika ya misaada yanakabiliwa na changamoto ya kusambaza vifaa katika eneo la Tigray nchini humo ambako majeshi ya serikali yamekuwa yakipigana na wapiganaji wa eneo hilo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Hakuna msafara wa chakula wa Umoja wa mataifa uliofika Tigray tangu katikati ya mwezi Disemba lakini WFP inasema magari makubwa 100 kwa siku yanahitajika kwa ajili yakuzuia njaa.

Katika tathmini yake ya karibuni ya usalama imegundua kwamba zaidi ya asilimia 80 ya familia walikuwa wana ukosefu wa chakula ikiwa chini ya theluthi moja wanapata kalori za kila siku wanazohitaji na katika mkoa wa Afar asilimia 28 ya Watoto chini ya miaka mitano wana utapiamlo na wako juu ya kiwango cha tahadhari cha umoja wa mataifa kwa asilimia 15.

WFP imesema kaskazini mwa Ethiopia watahitaji msaada wa chakula mwaka wote wa 2022, na inaziomba pande zinazohasimiana kuruhusu bidhaa kuingia.

Taarifa zinasema kuwa hata tathmini hiyo ya usalama imezingatia taarifa za Novemba mwaka jana.

XS
SM
MD
LG