Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:32

Shirika la haki za binadamu Amnesty International lawashutumu waasi wa Tigray

FILE - Mpiganaji wa vikosi maalum vya Afar akiwa Bisober, Tigray, Ethiopia, Dec. 9, 2020. Raia wasiopungua 20 wameuawa katika mapigano kati ya waasi na vikosi vinavyounga mkono serikali ya Ethiopia, huko Afar, kwa mujibu wa AFP July 22, 2021. Picha na AFP.

Ripoti mpya imetoa maelezo ya kina kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu kunakofanywa na wapiganaji kutoka mkoa wa Tigray nchini Ethiopia.

Ripoti hiyo iliyotolewa na shirika la haki za binadamu la Amnesty International imewashutumu waasi wa Tigray kutumia genge kuwabaka na kuwauwa kwa makusudi raia katika eneo jirani la Amhara.

Waasi hao walidhibiti eneo hilo kwa muda hadi pale waliposukumwa nyuma na vikosi vya serikali miezi miwili iliyopita.

Amnesty imesema waasi waliwauwa raia ambao hawakuwa na silaha katika mji wa Kobo na kuwanyanyasa kingono takriban wanawake 30 na wasichana katika kijiji cha Chena.

Mali za umma kama vile shule na hospitali ama viliibwa au kuharibiwa, taarifa imesema.

Tigray peoples liberation haikujibu kufuatia shutuma za karibuni lakini imekanusha shutuma kama hizo katika siku zilizopita. Serikali ya Ethiopia pia imeshutumiwa kwa mauaji na ubakaji.

XS
SM
MD
LG