Tuhuma hizo dhidi ya kampuni hiyo ya kubwa ya teknolojia ya Marekani inafuatia wiki iliyopita kugundulika makosa dhidi ya Apple ikiwa ni mara ya kwanza Brussels kutoa tuhuma rasmi chini ya Sheria ya Masoko ya Kidigitali ya EU (DMA).
Kesi hii ya hivi sasa inaangazia juu ya muundo wa usajili wa matangazo ya bure mapya ya Meta kwa ajili ya Facebook na Instagram, ambao umeibua malalamiko kadhaa kuhusu wasiwasi wa faragha ya watumiaji mitandao.
Mfumo wa “Malipo au idhini” wa Meta unamaanisha kuwa watumiaji wanatakiwa kulipia kuepuka takwimu kukusanywa, au wakubali kutoa takwimu zao kutumiwa na Facebook na Instagram ili waweze kutumia mitandao hiyo bure.
Umoja wa Ulaya ilisema imeitaarifu Meta kuhusu “maoni yake ya awali” kuwa muundo huo uliozinduliwa na kampuni hiyo mwaka jana “unakinzana” na DMA.