Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:01

Mahakama Kenya yaiamuru Sama kutowafukuza kazi wasimamizi wa maudhui


Miongoni mwa wasimamizi wa maudhui walikiokuwa wakifanya kazi na Facebook wakishaurian na wakili wao huko Nairobi, tarehe 12 Aprili 2023. Picha na Tony KARUMBA/AFP.
Miongoni mwa wasimamizi wa maudhui walikiokuwa wakifanya kazi na Facebook wakishaurian na wakili wao huko Nairobi, tarehe 12 Aprili 2023. Picha na Tony KARUMBA/AFP.

Mahakama ya Kenya siku ya Ijumaa iliamuru kusimamisha kufukuza kazi kwa wasimamizi wa maudhui kadhaa walioajiriwa na kampuni mkandarasi ya Sama inayofanya kazi na Meta, kampuni mama ya Facebook.

Makahama imeiagiza kampuni hiyo kubwa ya mitandao ya kijamii kutoa ushauri nasaha kwa wafanyakazi hao.

Jumla ya wasimamizi wa maudhui 184 walioajiriwa huko Nairobi na kampuni ya Sama, kampuni inayotumiwa na Meta kukidhi mahitaji ya wafanyakazi, waliwasilisha kesi mahakamani mwezi Machi, wakidai kufukuzwa kwao kazi ni "kinyume cha sheria".

Katika uamuzi wake wa kurasa 142, hakimu wa mahakama ya kazi, Byram Ongaya alisema kampuni ya Meta na Sama "zilizuiliwa kuvunja mikataba ya ajira" wakati ikisubiri kuamuliwa kwa kesi ya kupinga uhalali wa kuwafukuza kazi.

“Amri ya muda inatolewa inataka mikataba yoyote ambayo itamalizika kabla ya uamuzi kutolewa kuongezwa muda” mpaka hapo kesi hiyo itakapo malizika jaji huyo aliongeza.

Meta -- ambayo pia inamiliki Instagram na WhatsApp -- iliamriwa "kutoa huduma stahiki za afya na akili na kisaikolojia kwa walalamikaji na wasimamizi wengine wa maudhui ya Facebook".

Kampuni hiyo iliiambia mahakama kuwa ina nia ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Kampuni hiyo kubwa ya teknologia na yenye nguvu yenye makao yake makuu huko California, inashikilia kuwa haina uwepo rasmi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki na kwamba walalamikaji si waajiriwa wa Meta.

Kampuni hiyo pia inakabiliwa na kesi nyingine mbili nchini Kenya.

Mwaka 2022, aliyekuwa mfanyakazi wa Sama, raia kutoka Afrika Kusini, Daniel Motaung, alifungua mashitaka nchini Kenya dhidi ya ya kampuni hiyo ya Sama na Facebook, miongoni mwa madai yake ni pamoja na mazingira duni ya kazi na ukosefu wa msaada wa afya ya akili.

Kampuni hiyo kubwa inayomiliki mitandao ya kijamii, pia inakabiliwa na kesi nyingine nchini Kenya, ambapo raia wawili wa Ethiopia na shirika moja lisilo la kiserikali wanaishutumu Meta kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya matamshi ya chuki yaliyoko mtandaoni katika bara la Afrika.

Chanzo cha taarifa hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG