Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 07:19

App ya Threads yapata zaidi ya watumizi milioni 500 tangu kuzinduliwa kwake


Picha inayoonyesha ukurasa wa kwanza baada ya kufungua App ya Threads pamoja na nembo ya Meta.
Picha inayoonyesha ukurasa wa kwanza baada ya kufungua App ya Threads pamoja na nembo ya Meta.

App mpya ya Threads kutoka kampuni inayomiliki Facebook ya Meta na ambayo inashindana na Twitter imepata zaidi ya watumiaji milioni 500 ndani ya siku 5 tangu kuzinduliwa.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg amesema hayo Jumatatu na ikiwa na maana kwamba ndilo jukwaa linalokuwa kwa haraka zaidi. Tangu kuzinduliwa kwake Jumatano, Threads imepata watumiaji wa kila aina kuanzia wasanii, wanasiasa pamoja na watu wengine mashuhuri, ikionekana kuwa tishio kubwa zaidi kwa Elon Musk ambaye anamiliki Twitter.

Hata hivyo Threads ingali ina kibarua kigumu kwa kuwa Twitter tayari ina watumi aji karibu milioni 240 wanaolipia matumizi kulingana na ripoti ya kampuni hiyo Julai mwaka jana, kabla ya kununuliwa na Musk. Twitter imetishia kuishitaki Meta ikidai kwamba imetumia siri zake za kibiashara pamoja na taarifa za ndani kubuni app ya Threads. Wataalam wa sheria hata hivyo wanasema kwamba hilo huenda likawa gumu kulithibitisha.

Forum

XS
SM
MD
LG