Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 07:54

Mazungumzo kati wafanyakazi wa zamani na Facebook nchini Kenya yasambaratika


Nembo ya kampuni ya Facbook
Nembo ya kampuni ya Facbook

Wafanyakazi wa zamani wa Facebook nchini Kenya Jumatatu wamesema kwamba mazungumzo ya kusulihisha kesi waliyowasilisha dhidi ya kampuni inayomiliki Facebook, Meta yamesambaratika, na kwa hivyo huenda kesi mpya ikawasilishwa mahakamani.

Machi mwaka huu, wafanyakazi 184 waliyofutwa kazi na kampuni ya Sama, iliyopewa kandarasi na Meta waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa hatua hiyo ilikuwa kinyume cha sheria, na kwamba wafanyakazi wa Facebook nchini Kenya waliwekwa kwenye mazingira mabaya ya kikazi, wakati wakilazimishwa kufanya kazi pamoja na kunyimwa malipo mara kwa mara.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mazungumzo hayo yaliongozwa na jaji mkuu wa zamani nchini Kenya Willy Mutunga, pamoja na afisa kutoka wizara ya kazi, yalikuwa yamepangwa kuchukua siku 21 kuanzia Agosti 23.

Wakili wa wafanyakazi hao Mercy Mutemi amedai kwamba kampuni za Meta na Sama zinavuta muda, na wala hakuna ukweli kwenye mazungumzo hayo. Meta ambayo pia inamiliki Instagram, haijatoa tamko lolote kufikia sasa, kufuatia hatua hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG