EU yaunga mkono ombi la uanachama wa Ukraine, Moldova

Trans-Dniester, Odessa, Moldova, Crimea and Ukraine

Umoja wa Ulaya umeidhinisha  Ijumaa pendekezo la kuiruhusu Ukraine na jirani yake Moldova kuwa wagombea wa kujiunga na umoja huo, jambo ambalo litaleta mabadiliko makubwa ya kisiasa kutokana na uvamizi wa Russia.

Ukraine iliomba kujiunga na EU siku nne baada ya wanajeshi wa Russia kuvuka mpaka mwezi Februari.

Hivyo hivyo Moldova na Georgia, majimbo madogo ya uliokuwa Umoja wa Sovieti pia yanashindana pia na maeneo yanayotaka kujitenga yaliyokaliwa na wanajeshi wa Russia.

Mkuu wa tume ya utendaji ya EU Ursula von der Leyen alisema mjini Brussles kwamba, “Ukraine imebainisha wazi matarajio na azma ya nchi kuheshimu maadili na viwango vya Ulaya .”

Rais wa Ukraine Volodymir Zelenskyy alimshukuru Von De Leyen na wajumbe wa EU kupitia Twitter kwa uamuzi aliouita “ hatua ya kwanza ya uanachama wa EU ambayo kwa hakika itasababisha wapate ushindi karibuni.”

Naye Rais wa Moldova Maia Sandu alipongeza ishara hiyo uungaji mkono kwa Moldova na raia wake, na akasema alitegemea kuungwa mkono na nchi wanachama wa EU.

“Tuna nia ya dhati kufanya kazi kwa bidii,” alisema kwenye Twitter.

Wakati akipendekea hadhi ya ugombea kwa Ukraine na Moldova, tume hiyo haijasema kitu kuhusu Georgia, kwa vile ilisema bado kwanza inahitaji kutimiza baadhi ya masharti.