Russia hivi sasa inadhibiti takribani asilimia 80 ya mji wa viwanda mashariki mwa Ukraine wa Sievierodonetsk na imeharibu madaraja yote matatu ya kutoka mjini humo gavana wa eneo la Luhansk, Serhiy Haidai alisema Jumanne.
Kwa uharibifu wa madaraja uliofanywa na Russia, Haidai alikiri kwamba uhamishaji mkubwa wa raia kutoka Sievierodonetsk kwa sasa hauwezekani kwa sababu ya makombora na mapigano ya Moscow katika jiji hilo. Alisema vikosi vya Ukraine vimesukumwa hadi nje ya mji kwa sababu ya njia ya ardhini iliyoungua na silaha nzito zinazotumiwa na wa-Russia.
Lakini Haidai aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba vikosi vya Russia havijawazuia watu kuingia katika mji huo na kuiacha Ukraine na fursa ya kuwahamisha watu waliojeruhiwa, kuwa na mawasiliano na jeshi la Ukraine na wakaazi wa eneo hilo.