Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:04

Marekani yaitaka Russia kuheshimu haki za Wamarekani waliotekwa Ukraine


Picha za wanajeshi wawili wa Marekani waliostafu, Alexander Drueke na Andy Huynh waliotoweka nchini Ukraine, wakihofiwa kutekwa na wanajeshi wa Russia. Picha za Reuters na AP
Picha za wanajeshi wawili wa Marekani waliostafu, Alexander Drueke na Andy Huynh waliotoweka nchini Ukraine, wakihofiwa kutekwa na wanajeshi wa Russia. Picha za Reuters na AP

Marekani Alhamisi imeitaka Russia kuwachukilia Wamarekani wote wa kujitolea walioshikwa mateka wakati wakipigana upande wa wanajeshi wa Ukraine kama wafungwa wa vita, na kuheshimu haki zao za ubinadamu.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Mmarekani wa tatu anaaminika kutoweka nchini Ukraine mbali na wanajeshi hao wawili waliostaafu ambao waliripotiwa kutekwa na wanajeshi wa Russia katika mapambano makali wiki iliyopita.

"Warussia wana wajibu fulani na wanajeshi wa Ukraine ikiwemo wapiganaji wanaojitolea ambao wanaweza kuwa raia wa nchi nyingine waliojumuishwa katika jeshi wanapaswa kuchukuliwa kama wafungwa wa vita chini ya mikataba ya Geneva," msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price aliwambia waandishi wa habari.

Wafungwa wa vita lazima wapewe huduma na ulinzi unaolingana na hadhi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa kiubinadamu na kuheshimu haki zao za kimsingi za kujitetea mahakamani," alisema.

Familia na wabunge wa Marekani Jumatano walisema Alexander Drueke na Andy Huynh, wote wakiwa wanajeshi wa Marekani waliostafu ambao walikuwa wanaishi Alabama, walipoteza mawasiliano na jamaa zao wiki iliyopita wakipigana upande wa wanajeshi wa Ukraine karibu na mpaka wa Russia.

XS
SM
MD
LG