Russia iliwaambia wanajeshi wa Ukraine waliokuwa wamejificha kwenye kiwanda cha kemikali katika mji huo uliosambaratika kuacha upinzani usio na maana na kuweka silaha chini kuanzia Jumatano asubuhi, ikisistiza ni fursa nzuri katika vita vya kuwania udhibiti wa mashariki mwa Ukraine.
Watu wanaotaka kujitenga walinukuliwa na shirika la habari la RIA wakisema mipango iliyotangazwa na Moscow kufungua njia kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kufikishwa kwa raia waliokwama katika kiwanda hicho imevurugwa na mashambulizi ya Ukraine.
Ukraine imesema zaidi ya raia 500 ikiwemo watoto 40 wamekwamna pamoja na wanajeshi ndani ya kiwanda cha kemikali cha Azot ambako vikosi vyake vimezuia kwa wiki kadhaa mashambulizi ya Russia ambayo yamesababisha sehemu kubwa ya severodonesky kuwa magofu.