Katika hotuba yake ya video ya Jumamosi usiku , Zelenskyy alisema anajivunia Waukraine kuwarudisha nyuma warussia katika mkoa wa Donbas. "Kumbuka jinsi huko Russia mwanzoni mwa Mei, walitarajia kuikamata Donbas yote?" rais aliuliza kwa kejeli Jumamosi usiku.
Baada ya kushindwa kuikamata Kyiv, mji mkuu wa Ukraine, Moscow imejikita katika kuteka sehemu za eneo la mashariki lisiloshikiliwa na watu wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Moscow. Lakini badala ya kupata udhibiti wa haraka, vikosi vya Russia vimekabiliwa na vita vikali.