Nitaangalia kazi ya pamoja inayohitajika kwa ajili ya kujenga tena na hatua ambayo tayari imefikiwa na Ukraine katika kujiunga Ulaya,” amesema katika ujumbe wa Twitter.
Zelenskyy alisema Jumamosi nchi yake “bila shaka itashinda katika vita hivi ambavyo vimeanzishwa na Russia, akizungumza kutoka katika eneo lisilotajwa mjini Kyiv.
Katika hotuba iliyotolewa kwa wajumbe wa Kongamano la Shangri-La, mkutano wa usalama wa Asia unaofanyika hivi sasa Singapore, Zelenskyy alisema Ukraine inapambana kuendelea kusafirisha chakula kutokana na vita na baadhi ya sehemu za dunia zinakabiliwa “na mgogoro mkubwa sana wa chakula na njaa” kwa sababu ya Russia kuzingira maeneo ya Ukraine.
Siku ya Ijumaa, Rais Joe Biden alisisitiza kuwa taarifa za kijasusi za Marekani zilijaribu kuitahadharisha Ukraine juu ya hatari ya wazi ya uvamizi wa Russia lakini Zelenskyy “hakutaka kusikia hilo.”
Biden alitoa kauli hiyo wakati wa uchangishaji fedha huko Los Angeles ambako alikuwa anazungumzia kuhusu kazi yake ya kuhamasisha na kukusanya misaada kwa ajili ya Ukraine wakati vita ikiendelea katika mwezi wake wa nne.
“Kitu kama hiki hakijawahi kutokea tangu Vita vya Pili vya Dunia. Ninajua watu wengi walifikiria pengine nilikuwa na ongeza chumvi. Lakini nilijua tulikuwa na takwimu kusisitiza hili – akimaanisha Rais wa Russia Vladimir Putin – angeivamia nchi hiyo, kwa kuvuka mpaka.”
Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen amewasili mjini Kyiv Jumamosi kwa ajili ya kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kujadili kuijenga tena nchi hiyo na maendeleo ya uanachama wa Ukraine katika Umoja wa Ulaya ameeleza.