Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:59

Ukraine yakosoa wito wa Rais wa Ufaransa ukitaka Putin 'asidhalilishwe'


FILE - Kikosi cha wapiganaji wa kigeni wakujitolea kilichojiunga na jeshi la Ukraine kikijihami, wakati Russia ikiendeleza mashambulizi Ukraine katika mji wa Sievierodonetsk, mkoa wa Luhansk,Ukraine June 2, 2022.
FILE - Kikosi cha wapiganaji wa kigeni wakujitolea kilichojiunga na jeshi la Ukraine kikijihami, wakati Russia ikiendeleza mashambulizi Ukraine katika mji wa Sievierodonetsk, mkoa wa Luhansk,Ukraine June 2, 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amemkosoa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye mapema aliyasihi mataifa yenye nguvu duniani kuacha “kumdhalilisha” Rais wa Russia Vladimir Putin nchini Ukraine ili kuweka akiba nafasi ya suluhisho la kidiplomasia kwa mgogoro huo.

“Wito wa kuepuka kuid halilisha Russia unaweza tu kuidhalilisha Ufaransa na kila nchi nyingine ambayo itasema hivyo. Kwa sababu ni Russia ambayo inajidhalilisha yenyewe,” Kuleba aliandika ujumbe kwenye Twitter Jumamosi. “Sote ni vyema tulenge zaidi katika kuiweka Russia katika nafasi yake. Hili ndiyo litaleta amani na kuokoa maisha.”

“Hatupaswi kuidhalilisha Russia ili siku ikifika vita vitakaposimama, tuweze kujenga daraja la kutoka kupitia njia za kidiplomasia,” Macron alisema katika mahojiano ya Ijumaa na vyombo vya habari vya eneo, akiongeza kuwa Ufaransa itakuwa jukumu kuu la upatanishi.

Rais Emmanuel Macron
Rais Emmanuel Macron

“Nadhani, na nimemwambia yeye, kwamba amefanya kosa la kihistoria na la kimsingi kwa watu wake, kwake mwenyewe na kwa historia,” Macron alisema. “Nafikiri amejitenga mwenyewe. Na kujificha katika upweke ni jambo moja, lakini kutafuta njia ya kujitoa ni jambo gumu.”

Macron amekuwa akitafuta njia ya kuendeleza mazungumzo na Rais wa Russia Putin tangu Moscow ilipoivamia Ukraine mwezi Februari.

Msimamo wake umekosolewa mfululizo na baadhi ya washirika wa Ulaya Mashariki na Baltic, wakiona hilo ni kama kudumaza juhudi za kumshinikiza Putin kushiriki katika mashauriano.

Rais Emmanuel Macron (kulia) na Rais Vladimir Putin
Rais Emmanuel Macron (kulia) na Rais Vladimir Putin

Macron amezungumza na Putin mara kwa mara tangu uvamizi huo ikiwa ni sehemu ya juhudi mbalimbali za kufanikisha sitisho la mapigano na kuanza mashauriano ya dhati kati ya Kyiv na Moscow.

Ufaransa imeendelea kuiunga mkono Ukraine kijeshi na kifedha, lakini mpaka hivi sasa, Macron hajawahi kuipa Kyiv uungaji mkono wa kisiasa kama walivyofanya viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya, kitu ambacho Ukraine imekuwa ikimtaka afanye hivyo. Macron alisema hajafuta uwezekano wa kufaya ziara huko.

Katika matangazo ya televisheni mapema Jumamosi, gavana wa Luhansk Serhiy Haidai alisema majeshi ya Russia yalikuwa yanalipua madaraja yanayounganisha Mto Seversky Donets ili kuizuia Ukraine kupitisha vifaa vya kijeshi na misaada kwa raia katika mji wa Sievierodonetsk.

Haidai alisema jeshi la Ukraine linaendelea kushikilia sehemu walizozidhibiti ndani ya Sievierodonetsk na wamekuwa wakiyarejesha nyuma majeshi ya Russia katika maeneo mbalimbali.

Baadhi ya taarifa hizi zinatokana na chanzo cha habari cha shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG