Waziri wa ulinzi wa Ukraine amesema kwamba wanajeshi wake tayari wako kwenye mafunzo Ulaya, ya jinsi ya kutumia makombora yenye uwezo mkubwa wa kuharibu silaha za Russia.
Makombora hayo yametolewa na Marekani, na Uingereza na Ukraine ina matumaini kwamba yataisaidia katika vita hivyo.
Wakati Russia ilipoivamia Ukraine, ilikuwa na matumaini ya kushinda vita hivyo baada ya siku chache, lakini imekumbana na upinzani mkali kutoka kwa Ukraine, kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.
Wanajeshi wa Russia wanapigana kudhibithi mji mdogo wa viwanda wa Sieviero-donetsk, ambao ni lazima uwe chini ya udhibithi wake ili kushikilia kabisa mkoa wa Luhansk.
Pande zote katika vita hivyo zimepata hasara kubwa na wataalam wanasema kwamba vita hivyo vinaweza kudumu kwa muda mrefu.