Utafiti uliochapishwa Jumatano katika Jarida la Tiba la Uingereza ulisema watu walio ambukizwa na aina ya B.1.1.7 walikuwa kati ya asilimia 30 hadi 100 wana uwezekano wa kufa kuliko wengine walio ambukizwa na aina nyingine, na kiwango cha wastani karibu asilimia 64.
Tofauti ya B.1.1.7 imegunduliwa kuwa katika nchi zaidi ya 100 tangu vilipogunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi Septemba mwaka 2020 kusini mashariki mwa Uingereza.
Uchunguzi wa awali unaonyesha tofauti hiyo kuwa inaambukiza zaidi kuliko aina ya mwanzo.
Brazil ilitangaza vifo 2,286 vinavyotokana na Covid 19 Jumatano, idadi nyingine ya juu kwa siku moja ya vifo. Nchi hiyo ya Amerika Kusini inashughulika na kuongezeka kwa visa vya corona vinavyotokana na aina mpya ya P.1, ambayo iligunduliwa Novemba mwaka jana katikamji wa Manaus katika mkoa wa Amazonia.
Watafiti wanasema aina ya P.1 inaambukizwa mara 1.4 hadi 2.4 kuliko aina ya awali ya corona, na inaweza pia kuambukiza watu ambao tayari wamepona kutokana na COVID-19.