China imesema Ijumaa haitaitambua pasipoti ya Uingereza itakayo tolewa kwa wakazi wa Hong Kong kama cheti halali cha kusafiria au kitambulisho kuanzia Januari 31, 2020.
Tamko hilo limetolea na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian katika mkutano wa kila siku na waandishi wa Habari.
Hatua ya Beijing ya kuweka sheria mpya ya usalama wa taifa Hong Kong mwezi Juni 2020 ilipelekea Uingereza kutoa hifadhi ya ukimbizi kwa takriban wakazi millioni 3 wa Hong Kong.
Hifadhi hiyo ya ukimbizi watapewa wale wanaotimiza masharti ya kupewa passport ya Uingereza kuanzia Januari 31.