Blinken atangaza msaada wa dola milioni 134 kwa Wapalestina

Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza msaada wa dola milioni 135 zaidi kwa ajili ya wapalestina wakati wa ziara yake ya mashariki ya kati.

Blinken amewasili Qatar hii leo Alhamisi katika ziara yake ya kwanza nchini humo tangu Israel ilipomuua kiongozi wa kundi la wanamgambo la Hamas Yahya Sinwar.

Sinwar ambaye alikuwa adui mkubwa aliyekuwa akitafutwa sana na Israel.

Blinken amekutana na Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya Nje Mohammed bin Abduldahman Al Thani, mjini Doha.

Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim al-Thani

Wamezungumzia hali ya Gaza na namna ya kumaliza vita katika Mashariki ya Kati.

Qatar imekuwa mpatanishi muhimu wa Hamas, wakati Marekani ikijaribu kutafuta namna ya kumaliza vita kati ya Israel na wanagambo wa Hamas.