Biden alitarajiwa kuungana na maelfu ya watu kwa kumbukumbu ya kila mwaka kuhusu harakati za haki za kiraia ambazo zilipelekea kupitishwa kwa sheria ya kihistoria ya haki za kupiga kura karibu miaka 60 iliyopita.
Ziara ya Selma pia ni fursa kwa Biden kuzungumza moja kwa moja na kizazi cha sasa cha wanaharakati wa haki za kiraia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press (AP), Wamarekani wengi wanahisi kutoridhika kwa sababu Biden ameshindwa kutekeleza ahadi yake ya kampeni ya kuimarisha haki za upigaji kura na wanatamani kuona utawala wake ukiweka suala hilo katika uangalizi,
Biden anakusudia kutumia hotunba yake kusisitiza umuhimu wa kuadhimisha siku hiyo, ili historia isiweze kufutika, huku akitoa hoja kwamba kupigania haki za kupiga kura bado ni hatua muhimu katika azma ya kuleta haki za kiuchumi na haki za kiraia kwa Wamarekani Weusi, kulingana na maafisa wa White House.