Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 05:41

Clinton na Trump watoa hotuba kali North Carolina


Republican presidential candidate Donald Trump and Democratic presidential candidate Hillary Clinton at campaign rallies in North Carolina, Nov. 3, 2016.
Republican presidential candidate Donald Trump and Democratic presidential candidate Hillary Clinton at campaign rallies in North Carolina, Nov. 3, 2016.

Hillary Clinton na Donald Trump wamefanya mikutano sambaba za kampeni alhamisi usiku mjini North Carolina jimbo ambalo kila mmoja lazima ashinde kama wakitaka kwenda White house baada ya jumanne ijayo.

Mpinzani wa zamani wa Clinton katika chama cha Democrat Seneta Bernie Sanders alimtambulisha mgombea huyo huko Raleigh North Carolina wakati mpinzani wake Donald Trump alikuwa si mbali kutoka kwake akihutubia katika mkutano wa watu wengi wanaounga mkono jeshi huko Selma.

Wote walishambuliana kwa maneno ya kudhalilisha uwezo wa kila moja wao kufanya kazi huku kila moja akijaribu kuwavutia wapiga kura wake na kueleza huu ni wakati muhimu katika historia ya marekani.

Awali huko Greenville North Carolina, Clinton alionya kwamba Trump anaweza mbele maslahi yake na hajali nani ataumia. Clinton kwa mara nyengine anapata nguvu kutoka rais Barack Obama aliyekua Florida na washirika mwake wakuu kote nchini.

XS
SM
MD
LG