Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:49

Mshindi wa Grammy Nancy Wilson aaga dunia Marekani


 Nancy Wilson
Nancy Wilson

Mwimbaji mshindi wa tuzo ya Grammy Nancy Wilson amefariki akiwa na umri wa miaka 81.

Wilson, aliyestaafu kutoka shughuli za utalii mwaka 2011, amekufa jioni Alhamisi baada ya kuuguwa kwa muda mrefu nyumbani kwake huko mjini Pioneertown, katika Jimbo la California.

Wilson alikuwa anajiita kama mwana mitindo wa nyimbo badala ya muimbaji na alikuwa na namna ya kutengeneza nyimbo katika mtindo wa kipekee ili uwe ni wake na wakipekee.

Pengine nyimbo yake bora na ya mtindo wa kipekee zaidi ni “Guess Who I Saw Today,” (kisia nani nimekutana naye leo) katika onyesho lake lililokuwa limefaulu zaidi akieleza katika wimbo huo kuwa siku zote alikuwa na uvumilivu wa kumsubiri mpenzi wake kurudi nyumbani ili aweze kumsimulia yale yaliojiri katika siku yake.

Kwa upendo mkubwa anamuuliza mpenzi wake, “Unaweza kukisia nani nimemuona leo” baada ya kusimama “ katika mgahawa na baa yenye kuvutia zaidi kuliko zote nchini Ufaransa.

Anatumbuiza katika mwimbo wake akisema : Aliwaona watu wawili “wakipendana sana ikiwa ni dhahiri kwangu wakiwa chumbani.”

Halafu analeta mashara, akiuliza hilo tena na tena “Kisia nani nilimuona leo” na hatimaye na kwa mbwembwe anatoboa “ nimekuona wewe.”

Wilson pia alikuwa na kipaji cha maonyesho ya televisheni, filamu na radio. Baadhi ya kazi zake ni pamoja na “Hawaii Five O,” Police Story,” “the Robert Townsend spoof “Meteor Man na kwa miaka kadhaa alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Jazz cha Radio ya NPR, alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu, ikiwemo maandamano ya Selma ya mwaka 1965, na pia alipokea tuzo ya NAACP Image 1998.

Wilson aliwataja Nat King Cole, Dinah Washington na Jimmy Scott kwamba walichangia katika mafanikio yake.

Shirika la habari la Associate Press linaripoti kuwa kwa mujibu wa matakwa ya Wilson, hakutakuwa na ibada ya mazishi. Badala yake, sherehe ya kutambua mchango wake wakati wa uhai wake inawezekana ikafanyika Februari, mwezi wa siku yake ya kuzaliwa.

XS
SM
MD
LG