Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 10:34

Mwimbaji Aretha Franklin yuko mahtuti


Nyota wa muziki Aretha Franklin
Nyota wa muziki Aretha Franklin

Mwimbaji gwiji Aretha Franklin, nyota aliyewahi kushinda tuzo mbalimbali za Grammy, ni mgonjwa sana.

Aretha ambaye athari za muziki wake zinaenda miongo kadhaa nyuma, hali yake ni mahtuti na hivi sasa amezungukwa na wanafamilia, mwandishi mmoja ambaye ni rafiki wa familia yake ameandika hilo katika tovuti yake Jumatatu.

Franklin, Gwiji wa muziki wa Soul aliyejulikana kama “Queen of Soul” maarufu kwa muziki wake unaoitwa “Respect” (1967) na mwengine “I Say a Little Prayer” (1968), yuko taabani huko Detroit.

Familia yake inawaomba watu kumuombea na pia kuwapa fursa ya kuwa na faragha katika kumuuguza mgonjwa,” ameandika Roger Friedman katika tovuti ya Showbiz 411.

Franklin, ambaye aligunduliwa kuwa na saratani mwaka 2010, alitumbuiza Novemba 2017 katika hafla ilioandaliwa na taasisi ya Elton John AIDS Foundation huko New York.Onyesho lake la mwisho lilikuwa Philadelphia Agosti 2017.

“Onyesho lake lilikuwa lakuvutia kwani wakati huo tayari Aretha alikuwa akikabiliana na uchovu na kiu,” Friedman wrote, akieleza onyesho hilo la Philadelphia.

Katika kipindi chote cha kutumikia tasnia ya muziki aliweza kupata tuzo za Grammy 18, na moja ikiwa inatambua mchango wake wakati wote akiwa katika tasnia hiyo.

XS
SM
MD
LG