Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:58

Maandamano ya kibaguzi Marekani yashindwa kufikia malengo


Waandamanaji wanaopinga sera za kibaguzi wakiwa mjini Washington DC, Agosti 12, 2018.
Waandamanaji wanaopinga sera za kibaguzi wakiwa mjini Washington DC, Agosti 12, 2018.

Watu waliohudhuria mikutano wenye mvutano katika mji mkuu wa Marekani, Washington, Jumamosi na Jumapili hatimaye waliweza kusikika, ingawaje ujumbe wa pande hizo kinzani ulikuwa na tofauti kubwa.

Takriban dazeni mbili ya wazungu wenye sera za kibaguzi, wengine wakificha nyuso zao kwa vitambaa na bendera za Marekani, waliandamana katika viwanja vilivyoko pembeni ya mtaa ulioko karibu na White House Jumapili mchana lakini tukio hilo lilimalizika wakati mvua ikinyesha kabla ya muda uliopangwa wa kuanza maandamano hayo saa kumi na moja na nusu jioni.

Jason Kessler, mtu ambaye aliandaa shughuli hiyo kwa kuunga mkono “haki za kiraia za wazungu,” alitarajia watu kati ya 100 na 400 kuhudhuria, kwa mujibu wa kibali alichopewa kutoka kwa wasimamizi wa viwanja hivyo vya taifa.

“Ni sawa kwangu kushirikiana katika nchi hii na watu wengine kutoka duniani kote,” Kessler amesema, akiongoea kutoka katika jukwaa kabla ya mkutano huo kuanza rasmi, “ lakini iwapo unawaleta watu wengi mno mara moja, inakuwa siyo nchi ile tunayoijua na hili ndilo wanalofanya na ndio sababu wazungu wengi wanapata uchungu.”

Kessler pia amesema yeye sio mtu mwenye sera za kibaguzi. Waandishi wa habari waliwekwa mbali kabisa na mkutano huo na hawakuweza kuwauliza maswali washiriki wa maandamano hayo.

Kessler na kikundi chake cha waandamanaji waliwasili katika viwanja vya Lafayette na kuondoka mahali hapo chini ya usimamizi wa polisi.

Hata hivyo idadi yao ilikuwa imezidiwa na waandamanaji waliokuwa wanapinga sera za kibaguzi katika upande wa pili wa mkutano huo. Kuwepo kwa ulinzi mkali wa vyombo vya dola na uzio wa muda wa chuma, uliyatenganisha makundi hayo kutoweza kufikiana.

XS
SM
MD
LG