Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:49

Trump awataka Wamarekani kushikamana, wakati makundi kinzani yakiandamana


Meya wa Washington Muriel Bowser na mkuu wa idara ya polisi Peter Newsham wakijibu maswali kutoka kwa waandishi juu ya matayarisho ya maandamano yanayoongozwa na watu wenye misimamo mikali ya kibaguzi
Meya wa Washington Muriel Bowser na mkuu wa idara ya polisi Peter Newsham wakijibu maswali kutoka kwa waandishi juu ya matayarisho ya maandamano yanayoongozwa na watu wenye misimamo mikali ya kibaguzi

Mji mkuu wa Marekani, Washington na mji jirani wa jimbo la Virginia wanajiandaa Jumapili kushuhudia maandamano ya kuadhimisha mkutano mkubwa wa kwanza wa wazungu wenye sera za kibaguzi uliopelekea vurugu iliyo sababisha vifo huko Charlottesville, Virginia.

Waandamanaji wenye misimamo mikali ya kibaguzi na wale wanao wapinga wamejiandaa kufanya mikutano katika viwanja vilivyoko karibu na White House ambapo kutakuwa na ulinzi mkali. Ulinzi huo ni tahadhari iliyochukuliwa na vyombo vya dola kuepusha vurugu na uvunjifu wa amani.

Jason Kessler, aliyekuwa ameandaa mkutano wa Charlottesville ameahidi kufanya mkutano wa haki za “kiraia za watu weupe” baada ya utawala wa mji wa Charlottesville kuwakatalia kibali.

Wakati huo huo huko Charlotteville, kilomita 160 kuelekea kusini magharibi mwa Washington, maelfu ya watu wanategemewa kukusanyika kushuhudia kilichotokea mwaka jana na kuendeleza juhudi za kutafuta suluhu ya kuondosha ubaguzi katika taifa la Marekani.

Rais Donald Trump Jumamosi alitoa tamko akiwasihi wananchi kushikamana kama taifa moja.

“Lazima tushikamane pamoja kama taifa moja,” Trump aliandika katika ujumbe wake wa Twitter kutoka katika klabu yake ya mpira wa golf huko New Jersey. Nina laani kila aina ya ubaguzi na vitendo vya uvunjifu wa amani. Amani ni kwa sote Wamarekani!”

XS
SM
MD
LG