Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 10:41

Mchungaji Billy Graham azikwa


Franklin Graham, mwanaye Billy Graham, akihubiri wakati mjini Charlotte, North Carolina, Machi 2, 2018.
Franklin Graham, mwanaye Billy Graham, akihubiri wakati mjini Charlotte, North Carolina, Machi 2, 2018.

Mwili wa mwinjilisti maarufu Billy Graham ulizikwa siku ya Ijumaa nje ya maktaba iliyopewa jina lake katika mji wa Charlotee, North Carolina.

Jeneza la mhubiri huyo, ambalo lilibebwa na watoto wake, lilikuwa limetengenezwa na wafungwa katika jela la Louisiana State Penitentiary, maarufu kama "Angola."

Graham alizikwa kando mwa kaburi la mkewe.

Mazishi yake yalihudhuriwa na takriban watu 2,000, akiwemo rais Donald Trump, makamu wa rais Mike Pence, wake zao, familia ya mhubiri huyo na marafiki wa karibu.

Mmoja wa wanawe, Franklin Graham, alihubiri wakati wa ibada ya mwisho iliyofanyika kwenye maktaba hiyo.

Alisema hakukuwa tofauti kati ya Graham aliyejulikana na Wakristo kote duniani na yule aliyejulikana na familia.

Rais wa Marekani Donald Trump na makamu wake Mike Pence wakati wa mazishi ya mwinjilisti maarufu Billy Graham mjini Charlotte, N.C., March 2, 2018.
Rais wa Marekani Donald Trump na makamu wake Mike Pence wakati wa mazishi ya mwinjilisti maarufu Billy Graham mjini Charlotte, N.C., March 2, 2018.

"Billy Graham ambaye alionekana na mamilioni ya watu kwenye televisheni na viwanja mbalimbali ulimwenguni kote, ndiye Billy Graham tuliyemjua kama familia," alisema mwanawe amaye pia ni mchungaji.

Mchungaji Graham, ambaye alifariki dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 99, anaenziwa kwa kuwahubiria mamilioni ya watu duniani kote kwa njia ya mikutano ya injili na kupitia matangazo ya moja kwa moja ya redio na runinga.

Kwa zaidi ya wiki moja, Graham aliombolezwa kama mchungaji wa kipekee ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa hususan kwa Wamarekani, na aliyehubiria marais wa vizazi vingi wakati wa huduma yake ya miongo kadhaa.

Jeneza la mchungaji Billy Graham likiwa kwenye ukumbi wa bunge la Marekani, Capitol Rotunda, mjini Washington DC. Feb. 28, 2018.
Jeneza la mchungaji Billy Graham likiwa kwenye ukumbi wa bunge la Marekani, Capitol Rotunda, mjini Washington DC. Feb. 28, 2018.

Siku ya Jumatano, alikuwa mtu wa tano katika historia, kupewa heshima ya juu pale kwa mwili wake ulkipopelekwa kwenye ukumbi wa bunge la Marekani, Capitol Rotunda.

Mtu wa mwisho kutuniukiwa heshima hiyo, alikuwa ni mtetezi wa haki za watu weusi, Rosa Parks, ambaye alifariki dunia mnamo mwaka wa 2005.

Alipokuwa hai, Grahama alikuwa na mazoea ya kuwaambaia watu waliohudhuria mahubiri yake kwamba atakapokufa, atakuwa tu amebadilisha anwani na kuwataka wasihuzunike.

Kiongozi huyo alifanya maombi na kuwapa nasaha watu mashuhuri na wenye nguvu wa karne ya 21, tangu wakati wa utawala wa Rais Harry Truman mpaka Barack Obama.

Graham alikuwa kiongozi mwenye kuwavutia wengi, wataalamu wa dini wanasema, wakitaja kuwa ni kati ya wahubiri wachache wenye uwezo wa kuepuka udini na kuweza kuwafikia Wamarekani wengi.

Mnamo mwaka 1950, aliunda Umoja wa Wahubiri wa Billy Graham katika juhudi za kusambaza neno la Mungu kupitia kile kilichokuja kuwa maarufu hivi leo kama “crusades”, mahubiri ya mfululizo ambayo hufanyika katika viwanja mbalimbali.

Graham aliendesha mahubiri haya katika mabara yote isipokuwa Antarctica, akihubiri yeye mwenyewe kupitia matangazo ya satellite. Alihubiri katika mataifa ya Soviet kabla ya kuanguka kwa ukomunisti.

Na katika msimu wa baridi mwaka 1994, Billy Graham alitoa mahubiri huko China na Korea Kaskazini, ambako alikutana na viongozi wa kisiasa na kidini katika nchi hizo.

Kutokana na safari zake alizofanya katika mataifa mbali mbali ulimwenguni, mhubiri huyu mashuhuri wa Marekani alitoa fatwa kuwa Ukristo sio tu dini ya nchi za Magharibi.

“Ni wenye nguvu Afrika na Amerika ya kati na Asia kuliko ilivyo nchi za Ulaya, kwa hatua kubwa. Huko Ulaya , bado unaitwa Ukristo, lakini hauna ukakamavu na nguvu kubwa.

Na nilikuwa Rome na kufanya mazungumzo na Papa juu ya suala hili na nafikiri mtakubaliana na hilo – kwamba maisha halisi ya Ukristo hivi sasa yako kule tunakokuita ulimwengu wa tatu,” alisema.

XS
SM
MD
LG