George Michael, nyota wa muziki wa aina ya pop ambaye alifikia umaarufu akiwa na kikundi cha WHAM. Akiwa katika chati ya juu katika muziki ambao ulikonga mioyo ya mashabiki wake, aliweza kuthubutu kutoa maoni binafsi na ya kijamii, ameiaga dunia, msemaji wake alitangaza Jumapili. Mwanamuziki huyo amekufa akiwa na umri wa miaka 53.
Kikundi hicho cha WHAM kiliundwa na George Michael na Andrew Ridgeley mwaka 1981. Kwa kipindi kifupi walijulikana nchini Marekani kama WHAM UK kutokana na utata wa majina hayo kufanana na bendi ya Kimarekani.
Michael ameaga dunia akiwa nyumbani kwake huko Goring, England siku ya Jumapili. Msemaji wake, Cindi Berger, amesema hakuwa anaumwa. Meneja wa Michael, Michael Lippman amesema sababu ya kifo chake ni ugonjwa wa moyo. Familia yake imetoa tamko kupitia Kituo cha polisi cha Thames Valley ikieleza “alifariki katika hali ya amani nyumbani kwake wakati wa sherehe za krismasi.”
“Familia yake wanaomba faragha wakati huu mgumu na wa huzuni. Hakutakuwa na tamko jingine kwa wakati huu.”
Kabla ya Lippmann’s kutoa tangazo hili, polisi walitoa tamko wakisema kifo cha mwanamziki huyu “ hakina maelezo lakini hakuna kinachoshukiwa” na kuwa “ uchunguzi wa kutambua sababu ya kifo utafanywa mara moja.”
Pengo la Michael linaendeleza majonzi yaliyoukumba ulimwengu wa muziki, ambapo David Bowie, Prince na Glenn Frey wakiwa ni kati ya wale ambao wamekufa kabla ya kufikia miaka 70.
Akiwa ni mwanamuziki aliye simama peke yake, aliweza kukua kimuziki, alikuwa mwimbaji na mwandishi mahiri wa nyimbo, ambaye wapinzani wake walimsifia kwa uwezo wake wa kuimba na kusherehesha maudhui ya muziki. Aliweza kuuza takriban zaidi ya albam milioni 100 duniani kote. Pia alitunukiwa tuzo mbalimbali za Grammy na American Music Awards, na kurekodi albam zake pamoja na wanamuziki wakongwe kama vile Aretha Franklin, Ray Charles, Luciano Pavarotti na Elton John na wengine.
“Nimepoteza rafiki kipenzi- mkarimu, mwenye moyo mkunjufu na mwanamziki mahiri,” Elton John aliandika katika mtandao wake wa Instagram.
Alifikia mafanikio makubwa lakini hakupenda kuwa maarufu. Alizungumzia kupunguza ziara zake na mahojiano na kutaka kazi zake zijitangaze zenyewe. Moja katika masupasta alifikiria kuwa alichofanya ni ujinga: katika barua ya wazi Septemba 9 1990, Frank Sinatra alimshauri Michael “ hebu bwana jiachie” na kubadilika.”
“Lakini balaa la umaarufu ni pale hakuna anayetokea katika shoo zako na wewe unamwimbia mhudumu katika sehemu ya starehe iliyotupu ambayo haijapata mteja tokea zama za mtakatifu Swithin’s day,” Sinatra aliandika.
Michael, ambaye ni mtanashati na mwenye kumudu jukwaa, alianzisha umoja wa WHAM na rafiki yake wa siku nyingi Andrew Ridgeley mwanzoni mwa miaka ya 80. Akisaidiwa na MTV, ambayo pia ilianzishwa wakati huohuo, alivuka kwa urahisi Atlantic kuja kupata umaarufu Marekani pamoja na Michael, akiwa ni mwimbaji mkuu, kwa kawaida ndio kivutio kikubwa.
Alianza usanii akiwa peke yake kabla ya WHAM akajitenga tena, baada ya kibao chake kilichopata umaarufu mkubwa “Careless Whisper,” iliyoendelea kutamba. Wapinzani wake kwa jumla waliangalia nyimbo zake wakati yuko na WHAM ni zenye mvuto lakini zenye kufifia katika ulimwengu wa muziki wa aina ya pop na hata hivyi kumpa juhudi za kipekee na maksi za juu.
Katika kipindi chake cha uanamuziki, tatizo lake la kutumia madawa na majaribio yake hatarishi katika ngono yalimwingiza mara nyingi katika matatizo ya kisheria, hasa lile maarufu la mwaka 1998 alipokamatwa kwa kitendo cha aibu katika eneo la hadhara mjini Los Angeles.
Hata hivyo aliweza kuligeuza tukio hilo katika muziki uliokuja kuwa maarufu ambao uliwasukuma wapenzi wa muziki wake kufurahia kitendo chake, na pia kukiri kwake kuwa yeye ni shoga kwa wakati ule kilimpa umaarufu zaidi.