Biden akutana na wanajeshi wa Marekani Poland

Rais Joe Biden awatembelea wanajeshi wa Marekani Ijumaa, March 25, 2022, mjini Jasionka, Poland. (AP Photo/Evan Vucci)

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na kuwasikiliza wanajeshi wa Marekani walio kwenye mpaka wa Poland na Ukraine katika juhudi za kutaka kufahamu zaidi kuhusu hali ya kibinadamu ya mamilioni ya wakimbizi wanaotoka Ukraine na kuingia Poland kutokana na uvamizi wa Russia.

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na kuwasikiliza wanajeshi wa Marekani walio kwenye mpaka wa Poland na Ukraine katika juhudi za kutaka kufahamu zaidi kuhusu hali ya kibinadamu ya mamilioni ya wakimbizi wanaotoka Ukraine na kuingia Poland kutokana na uvamizi wa Russia.

Biden amekutana na kikosi cha jeshi la Marekani kinachoshirikiana na wanajeshi wa Poland.

Anatarajiwa kusafiri hadi Warsaw Jumamosi kwa mazungumzo na rais wa Poland Andrzej Duda.

Umoja wa Ulaya umesema wkamba karibu watu milioni 3.5, nusu yao wakiwa watoto, wamekimbia vita nchini Ukraine, na zaidi ya milioni 2.2 wameingina Poland.

Msemaji wa serikali ya Russia Dmitry Peskov, amesema kwamba hakuna kitu kibaya kitatokea iwapo Marekani na washirika wake watafanikiwa kuiondoa Russia kati ya nchi 20 zenye nguvu sana za kiuchumi duniani, kwa sababu idadi kubwa ya nchi hizo tayari zina ushindani mkubwa wa kiuchumi na Moscow.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amekataa ombi la rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy la kutaka Hungary kuunga mkono vikwazo vya kutonunua mafuta kutoka Russia, akisema kwamba ombi la Zelensky halijatilia maanani maslahi ya Hungary na kwamba hatua hiyo itavuruga uchumi wa Hungary.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ni mshirika mkubwa wa rais wa Russia Vladmir Putin.

Hungary ndio nchi pekee katika Umoja wa Ulaya inayopakana na Ukraine, ambayo imekataa kutoa msaada wa silaha kwa Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Russia.