Biden akubali kimsingi kufanya mazungumzo na Putin

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Russia Vladimir Putin

Rais wa Marekani Joe Biden amekubali kimsingi kufanya mkutano na rais wa Russia Valdmir Putin kujadili kuhusu mzozo wa Ukraine.

Mazungumzo hayo yaliyopendekezwa na Ufaransa yatafanyika kama Russia haitomvamia jirani yake, white house imesema.

Hata hivyo Kremlin imesema hakuna mipango yenye nguvu kwa ajili ya mkutano huo.

Inatarajia kwamba mazungumzo kama hayo yanaweza kupelekea suluhu ya kidiplomasia katika mzozo wa kiusalama unaoonekana kuwa mbaya zaidi katika bara la Ulaya kwa miongo kadhaa.

Maafisa wa kijasusi wa marekani wanasema kuna uwezekano mkubwa Russia kuanza operesheni za kijeshi, ambapo Moscow imekanusha. Tangazo la mkutano huo lilitolewa na rais wa ufaransa Emmanuel Macron baada ya kuzungumza na rais wa Russia Vladimir Puttin kwa njia ya simu kwa takriba saa tatu.

Baada ya hapo Jumatatu Rais Macron alizungumza na rais Biden kwa dakika 15.

Hata hivyo ofisi ya Macron imesema maelezo ya kina kuhusu uwezekano wa mkutano huo yatajadiliwa wakati wa mkutano baina ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov siku ya Alhamisi.