Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 17:41

Mashambulizi ya mabomu, mizinga yaongezeka Donbas huku wingu la vita likitanda


Mwanajeshi wa Jeshi la Ukrainian akipita mbele ya nyumba iliyoharibiwa na waasi wanaoungwa mkono na Russia mjini Mariinka, mkoa wa Donetsk re Februari 7, 2022. (Photo by Aleksey Filippov / AFP)
Mwanajeshi wa Jeshi la Ukrainian akipita mbele ya nyumba iliyoharibiwa na waasi wanaoungwa mkono na Russia mjini Mariinka, mkoa wa Donetsk re Februari 7, 2022. (Photo by Aleksey Filippov / AFP)

Na katika tukio lenye kushtua, Rais wa Russia Vladimir Putin amesaini amri ya kiutendaji Jumamosi akiwataka wanajeshi waliostaafu kurudi kwenye mafunzo na mazoezi.

Mabomu na mizinga imeendelea kupigwa usiku wa kuamkia Jumamosi mkoa wa Donbas, mashariki mwa Ukraine, huku mashambulizi mazito ya mabomu yakizusha hofu kuwa mapambano ya kijeshi yanaweza kuanza.

Mkuu wa jamhuri ya Donetsk iliyotangaza kujitawala Jumamosi alitoa amri ya kuwahamasisha wanaume wote wenye afya nzuri kuripoti kwa “makamisaa wa jeshi” kujiandikisha na wanamgambo wa eneo lao.

Wanaume wenye umri wa miaka 18 na 55 pia wanazuiliwa kuondoka jamhuri yenye mtindo wake wa kujitawala inayoungwa mkono na Russia iliyoko katika ukingo wa mashariki mwa Ukraine.

Na katika tukio lenye kushtua, Rais wa Russia Vladimir Putin amesaini amri ya kiutendaji Jumamosi akiwataka wanajeshi waliostaafu kurudi kwenye mafunzo na mazoezi.

Baadhi ya wachambuzi wanaeleza hili ni tukio la kila mwaka, lakini kwa kawaida linafanyika mwezi Aprili, na siyo Februari. Yevhen Fedchenko, mwanazuoni wa Ukraine anayetafiti masuala ya habari potofu, anasema, “ni nyenzo moja ya ziada ya kupandikiza hali ya utata.”

Taasisi ya Usalama na Ushirikiano ya Ulaya imeripoti Jumamosi kukiukwa mara kwa mara kwa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2015 huko Donbas kuliko ilivyokuwa Februari 12.

Sehemu ya eneo la Donbas, ambalo linajumuisha jamhuri iliyojitangaza kujitawala ya Luhansk, zimekuwa ni wazi zinakaliwa kwa mabavu na Russia kwa miaka nane iliyopita.

OSCE imeripoti ukiukaji zaidi wa makubaliano eneo ya Luhansk kuliko Donetsk kwa siku mbili zilizopita, na hata hivyo, waangalizi wa muda mrefu wanasema upigaji mabomu katika eneo hilo na linaloizunguka Donetsk umeongezeka zaidi walivyoshuhudia kwa miaka mingi.

Ijumaa, viongozi waasi wanaoungwa mkono na Moscow, ambao Ukraine inawaona ni wasaliti wa Kremlin, waliamuru kuondolewa kwa idadi kubwa ya raia katika video zilizowekwa katika mitandao, wakisema jeshi la Ukraine linaandaa mashambulizi – shutuma ambazo Kyiv imekanusha vikali.

XS
SM
MD
LG