Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 16:37

Putin, washirika wake na taasisi za Russia zitalengwa na vikwazo vya Uingereza


Chensela wa Ujerumani Olaf Scholz, na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson wakiwa pamoja kabla ya Mkutano wa Kiusalama wa Munich kuanza mjini Munich, Ujerumani Februari 19, 2022. Matt Dunham/Pool via REUTERS
Chensela wa Ujerumani Olaf Scholz, na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson wakiwa pamoja kabla ya Mkutano wa Kiusalama wa Munich kuanza mjini Munich, Ujerumani Februari 19, 2022. Matt Dunham/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema Jumapili kuwa Uingereza itatumia vikwazo vikali sana “vinavyowezekana ” vya kiuchumi dhidi ya Russia iwapo itaivamia Ukraine.

Johnson ameiambia BBC vikwazo hivyo havitamlenga Rais wa Russia Vladimir Putin peke yake na washirika wake, “ lakini pia vitalenga makampuni na taasisi ambazo kimkakati ni muhimu kwa Russia.”

Kiongozi huyo wa Uingereza alisema, “Tutayazuia makampuni ya Russia kuongeza mapato yao katika masoko ya Uingereza, na tuko pamoja na marafiki zetu wa Marekani katika hatua ya kusitisha biashara kwa sarafu ya paundi na dola.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Putin walizungumza kwa simu Jumapili asubuhi na Ikulu ya Elysee imeeleza kuwa “ni hatua ya mwisho na juhudi muhimu za kuzuia mgogoro mkubwa huko Ukraine.

Mazungumzo hayo yamekuja wiki mbili baada ya kiongozi huyo wa Ufaransa kwenda Moscow kumsihi Putin kutoivamia Ukraine.

“Ni lazima tumzuie Putin kwa sababu hataacha akisha kuivamia Ukraine tu,” Liz Truss, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, alisema katika mahojiano ya Jumapili na gazeti la Daily Mail juu ya hali iliyowazi ya uvamizi wa Ukraine.

“Putin amesema haya yote hadharani, kuwa anataka kuunda Russia iliyo na nguvu zaidi, anataka kurejea katika hali kama iliyokuwa hapo awali ambapo Russia ilikuwa inadhibiti eneo kubwa la Ulaya Mashariki.”

Ursula von der Leyen, mkuu wa Tume ya Utendaji ya Umoja wa Ulaya, alisema, “Fikra hizo za Kremlin hatari, zinazokuja kutoka katika kiza cha siku za nyuma, zinaweza kuigharimu Russia mafanikio yake ya siku za usoni.

Kiongozi huyo amesema iwapo Russia itaivamia Ukraine, Russia itakuwa imejizuilia kufikia masoko ya fedha na bidhaa za teknolojia, kwa mujibu wa vikwazo vinavyo andaliwa.

XS
SM
MD
LG