Biden aitaja Kenya kama mshirika mkuu wa Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Kenya William Ruto wakielekea kwenye mkutano Oval Office, Alhamis Mei 23, 2024. Picha na Evan Vucci/Pool via REUTERS

Hatua ya Biden kuitaja Kenya kama Mshirika mkuu ambaye si mwanachama wa NATO inafanyika wakati Kenya inajitayarisha kupeleka maafisa wake Haiti kuongoza kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachopelekwa kujaribu kurudisha utulivu na kukabiliana na mzozo wa usalama katika taifa hilo la Caribean.

Rais Biden alimkaribisha mgeni wake Ruto wa Kenya katika Ikulu Jumatano na walizungum zaidi juu ya namna ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao, pamoja na nafasi za uwekezaji katika Nyanja mbali mbali za teknolojia kati yao.

Rais Biden alizungumzia juu ya nafasi za ushirikiano na ubunifu kutoka Sillicon Valley kuelekea Silicon Savanah akimaanisha vituo vikuu vya teknolojia katika nchi zote mbili Marekani na Kenya.

Rais Biden alisema “Tunazindua enzi mpya ya teknolojia, ushirikiano wa kiteknolojia kati ya Kenya na Marekani ikiwa ni pamoja na kubadilishana na uwekezaji katika Nyanja nyeti za usalama wa mitandao, akili membe na vifaa vya komputa”

Rais Ruto akisisitiza kwamba rais wa Kenya ndio washirika wanaostahiki wa tehnolojia, uwekezaji na mtaji wa Marekani

Naye rais Ruto alisema “Vijana wetu wenye vipaji, elimu, ubunifu na teknolojia ya kisasa kabisa ya kimarekani na mtaji wa uwekezaji na wawekezaji ambao wanahamu ya kupoata nafasi sio tu nchini Kenya lakini kwenye bara zima ni mambo yanaoingilian kabisa kwa wakati huu.”

Ziara hii ya kwanza ya kitaifa kufanywa na kiongozi wa nchi ya kiafrika katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 inasherekea pia ushirikiano na uhusiano wa miaka 60 kati ya Marekani na Kenya.

“Leo tunapoadhimisha miaka 60 ya uhusiano kati ya nchi zetu , ni wazi wananchi wetu ndio nguvu halisi ya ushirikiano na ushirikiano ambao unafanyakazi vyema. Hakuna Nyanja iliyonawiri kama upande wa ubunifu na ndio maana tuna mambo mengi kwenye meza ya mazungumzo,” alisema Rais Biden

Alhamis viongozi hao wataendelea na mazungumzo na mikataba ya ushirikiano ikitazamiwa kutiwa saini.