Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 22:35

Mzozo wa Haiti kuwa kipaumbele katika mkutano baina ya Biden na Ruto.


Rais wa Kenya William Ruto akiwa na mkewe Rachel Ruto walipowasili Marekani kwa ajili ya ziara ya siku tatu. Picha kwa hisani ya serikali ya Kenya.
Rais wa Kenya William Ruto akiwa na mkewe Rachel Ruto walipowasili Marekani kwa ajili ya ziara ya siku tatu. Picha kwa hisani ya serikali ya Kenya.

Rais wa Kenya William Ruto atakutana na Rais Joe Biden wa Marekani mjini Washington wiki hii, wakati mzozo wa Haiti na juhudi za kuimarisha biashara kati ya nchi zao vinatarajiwa kuwa juu katika agenda ya mazungumzo yao.

Ikitajwa kama ziara ya kihistoria na ofisi ya Ruto, hii ni ziara ya kwanza rasmi ya kitaifa ya rais wa kenya hapa Marekani baada ya miongo miwili na ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika tangu mwaka 2008.

Mazungumzo ya Biden na Ruto siku ya Alhamisi yatazingatia zaidi ushirikiano wa kibiashara na usalama ikiwemo ahadi ya Kenya kuongoza kikosi cha kimataifa kinachoungwa mkono na UN kwa ajili ya kutaka kutatua mzozo wa Haiti na kuirejesha katika utawala wa kisheria baada ya ghasia zinazosababishwa na magenge ya uhalifu.

Mapema mwaka huu msemaji wa White house Karine Jean Pierre alisema ziara hii itaimarisha nia ya dhati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kufikia amani na usalama na kupanua ushirikiano wa kiuchumi, na kusimama pamoja katika kutetea demokrasia.

Kenya iliahidi kupeleka maafisa wa polisi 1, 000 ili kuongoza maafisa wa polisi kutoka nchi nyingine huko Haiti, ingawa Marekani na mataifa mengine makubwa yamekataa kupeleka maafisa wao huko Haiti.

Rais Ruto aliwasili Atlanta Georgia Jumatatu ambako amekua na mikutano mbali mbali na wakuu wa jimbo, mashirika ya maendeleo na Wakenya wanaoishi katika mji huo. Moja kati ya hotuba zake muhiumu huko Atlanta ilikua ni juu ya uwongozi na demokrasia kwenye kituo cha Carter Center.

Forum

XS
SM
MD
LG