Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:40

Rais wa Kenya ameitisha mkutano maalum wa baraza la mawaziri


Rais wa Kenya, William Ruto
Rais wa Kenya, William Ruto

Mvua zimesababisha vifo vya watu  takriban 170 na wengine 185,000 kukoseshwa makazi tangu mwezi Machi, ofisi ya rais imesema.

Rais wa Kenya William Ruto ameitisha mkutano maalum wa baraza la mawaziri siku ya Jumanne kujadili hatua za kukabiliana na mafuriko mabaya sana ambayo yamesababisha vifo vya watu takriban 170 na wengine 185,000 kukoseshwa makazi tangu mwezi Machi, ofisi ya rais imesema.

Mvua kubwa kuliko kawaida za masika zikichanganyika mwendeleo wa hali ya hewa ya El Nino, zimeiharibu nchi hiyo ya Afrika Mashariki, na kuteketeza vijiji pamoja na kutishia kusababisha uharibifu zaidi katika wiki zijazo.

Katika tukio moja baya sana ambalo lililowaua wanavijiji karibu 50, bwawa la muda lilipasuka huko Rift Valley kabla ya alfajiri ya Jumatatu, na kusababisha mtiririko wa maji na matope kuteremka chini ya kilima na kumeza kila kitu.

Janga hilo ndiyo baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu kuanza kwa msimu wa mvua. Hadi sasa watu 169 wamefariki dunia kutokana na mafuriko kulingana na takwimu za serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG