Biden aibuka tena kidedea uchaguzi mwengine wa 'Super Tuesday'

Joe Biden (kulia) na Bernie Sanders

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, amepata ashindi mkubwa katika uchaguzi wa awali wa kumtafuta mgombea wa chama cha Democratiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba 2020.

Makamu Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, amepata ashindi mkubwa katika uchaguzi wa awali wa kumtafuta mgombea wa chama cha Demokratiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba 2020.

Biden ameshinda katika majimbo manne likiwemo Michigan, na kujiweka katika nafasi nzuri sana na kushinda uchaguzi huo wenye kinyang'anyiro kikali kati yake na Seneta Bernie Sanders.

Ushindi huo, tayari unamuweka Biden, mwenye umri wa miaka 77, katika nafasi ya kushinda tiketi ya chama hicho na kukabiliana na Rais Donald Trump wa chama cha Republican, katika uchaguzi wa Novemba tarehe 3 mwaka huu.

Biden, ameeleza matumaini ya kupata uteuzi wa chama, na kutoa mwito wa chama kuungana pamoja kwa kuunganisha nguvu na wafuasi wa Sanders.

Kulingana na ukusanyaji wa maoni baada ya kupigwa kura, ushindi wa Biden katika majimbo ya Michigan, Mizuri, Missisipi na Aidaho, ulihusisha uungwaji mkono kutoka kwa wafuasi wake wakiwemo wanawake, Wamarekani weusi, wanafunzi, watu wenye umri mkubwa, wanachama wa muungano ya wafanyakazi.

Tukio la Sanders kushindwa katika majimbo aliyoshinda mwaka 2016, linamuongezea shinikizo kubwa la kumtaka ajiondoe kwenye kinyang’anyiro hicho ili kutoa nafasi nzuri kwa Wademokrat kujiandaa kukabiliana na Rais Donald Trump.

Sanders, hajatoa taarifa yoyote baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Jumanne. Kwa kawaida, hutoa taarifa baada ya matokeo kutolewa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.