Uchaguzi mkuu wa taifa wa Mei 29 unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kuwahi kutokea, utafiti ukipendekeza kuwa chama cha ANC kitashinda chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza tangu demorasia ianze mwaka 1994.
Sasa, chama cha upinzani kinachoitwa uMkhonto weSizwe, au MK kwa kifupi , kimeikasirisha ANC kwa kujipa jina linalotokana na kitengo cha kijeshi cha ANC ambacho kilipigwa marufuku, kiliundwa na Nelson mandela na kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Rais wa zamani Jacob Zuma, shujaa wa ANC, amekiunga mkono chama cha upinzani na kuongeza majeraha tu, na ANC kimemsimamisha.
Jumatatu, ANC ilikwenda katika makahama ya uchaguzi kwa madai kuwa chama cha MK hakikukamilisha vipengele muhimu wakati wa kujisajili kwenye tume ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana.