Bado hazijakwisha wakati mvua zaidi zinatarajiwa mpaka mwezi Juni. Mwandishi wa VOA Nairobi, Mariama Diallo anaripoti.
Katika shule ya msingi ya Mathare North, Beatrice Achieng amekuwa akitayarisha chakula kwa wiki mbili zilizopita kwa ajili ya mamia ya waathirika wa mafuriko ambao wamepatiwa hifadhi katika kambi hii ya Watu Wasiokuwa na Makazi Ndani ya Nchi.
Anafanyia shughuli zake katika shirika la hisani la Tushinde Children’s Trust, ambalo lina operesheni zake katika makazi yasiyo rasmi ya Mathare na Kiambiu jijini Nairobi.
Beatrice Achieng, Tushinde Children’s Trust anaeleza: “Kuna takriban watu 300 wanaoishi hapa na mimi nina uwezo wa kuwalisha 200. Kuna taasisi ya serikali ya kaunti inayoleta chakula inaitwa Dishi na County, wao pia wanatusaidia chakula.”
Monikah Musyoka alifika hapa baada ya kupoteza nyumba yake katika mafuriko ya karibuni. Watoto wake wanne hawawezi kwenda shule kwa vile zimefungwa kwa muda usiojulikana.
Monikah Musyoka, Muathirika wa Mafuriko anasema: “Tuna matumaini kuwa serikali itatusaidia vitabu, kujenga madarasa ili watoto wetu waweze kurejea shule na kuendelea na masomo.”
Wiki hii, Rais wa Kenya, William Rutto, alitembelea eneo la Mathare, na kusema dola milioni 7,.6 zitatumika kujenga tena shule zote ambazo zimeathiriwa na mafuriko, kabla ya kufunguliwa tena.
Pia, utawala wake unapanga kuwalipa fidia waathirika kwa miezi mitatu..
William S. Ruto, Rais wa Kenya anasema: Huko kwenye kambi, muathirika mwingine, Felkix Ocheng, alitueleza ilikuwa saa nne usiku wakati maji yalipoanza kutiririka na kuingia nyumbani kwake wiki mbili zilizopita. Anasema wakati sehemu hii si muafaka, hana kwingine kwa kwenda.
Felix Ocheng, Muathirika wa Mafuriko: Katika eneo la Mathari, baadhi ya nyumba zimejenga kwenye kingo za mto nazo tayari zimeanguka
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Hali ya Hewa, David Gikungu anasema matukio ya wiki zilizopita yamevuka kituo chochote ambacho kilipelekea mafuriko ya mwaka jana yaliyosababishwa na hali ya hewa ya El Nino, ambayo anaelezea inaendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwa kile ambacho kinatokea hivi sasa.
Kwasababu ya hilo anasema, ni vigumu kubashiri wakati mvua zitaanza kupungua.
David Gikungu, Huduma za Hali ya Hewa Kenya: “Nimezungumzia Aprili kama kilele kwasababu hiyo ilikuwa na kawaida – Machi, Aprili, Mei – na Aprili kwa kawaida kunakuwa na mvua kubwa zaidi. Tunataka kuona ikiwa hizi zinaweza kuwa na ushawishi katika msimu huu wa 2024, bado itakuwa kilele au ikiwa bado zitashuka.”
Wakati huo huo, Peter Murgor, Meneja wa Msalaba Mwekundu Kenya katika Kitengo cha Kupunguza Hatari za Maafa, anasema kinachotokea katika nchi jirani pia kinaiathiri moja kwa moja Kenya.
Peter Murgor, Chama cha Msalaba Mwekundu Kenya:“Jana tulikuwa na jambo fulani huko katika mkoa wa kaskazini ambako moja ya masoko yameharibika kwasababu ya mvua huko Uganda. Huko kaskazini, katika mikoa ya nyanda za juu mashariki, ambako kuna mvua kubwa nchini Ethiopia, kuna mafuriko Kenya. Na hivyo hivyo kwenye mpaka wa Somalia na Tanzania.”
Pia anasema watu wengi zaidi huenda wakakoseshwa makazi kama mabwawa zaidi yatajaa maji.
Murgor ameongeza kuwa: “Sehemu kama Tana River, bado wana masuala kadhaa, dharura, sehemu kama zile za nyanda za chini Magharibi mwa Kenya, Homabay, kaunti ambazo zinazunguka eneo la Ziwa, maji huko Ziwa Victoria, ambayo kwa kweli yamejaa mno.”
Kwa sasa, ni vyema kuwa na mwamvuli, utabiri wa hali ya hewa wiki hii unasema mvua bado zinatarajiwa katika sehemu nyingi za nchi. Lakini dhoruba haitakuwa kubwa kama ilivyoshuhudiwa siku za karibuni.