Shirika la Hali ya Hewa Duniani linaonya kuwa kimbunga Hidaya, ambacho kinatarajiwa kutua nchini Tanzania na Kenya wikiendi hii, kinatishia kuzidisha mgogoro wa kibinadamu unaosababishwa na mvua kubwa katika nchi hizi na nyingine ambazo zilipata mafuriko makubwa katika Afrika Mashariki.
“Hidaya ni mfumo wa kwanza uliorekodiwa kufikia kiwango cha kimbunga cha tropiki katika sehemu hii ya dunia. Hatuzungumzii kuhusu Sudan. Tunazungumza kuhusu maeneo ya mnyanda za chini na Afrika Mashariki,” msemaji wa WMO, Clare Nullis aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva siku ya Ijumaa.
Ni muhimu kihistoria. Pia kitakuwa na athari kubwa sana, na hasa kwa Tanzania, ambapo ardhi tayari imejaa maji. Tanzania ambayo imeathiriwa na mafuriko, intarajiwa kupigwa tena na mvua kubwa zaidi zinazonyesha kutoka kwa mfumo huu.
Forum