Gavana wa Jimbo la Maryland, Wes Moore, ameweka wazi kuwa hapakuwa na kitendo chochote cha kigaidi baada ya daraja kuu katika mji wa Baltimore kubomoka Jumanne asubuhi wakati meli iliyobeba mizigo kugonga nguzo yake.
Moore alisema uchunguzi wa awali ulionyesha ni tukio la “ajali” na hapakuwa na “ushahidi wa kutegemewa kuwepo shambulizi la kigaidi.” Aliahidi kutoa fedha na kuwashukuru waokoaji kwa moyo wao.
Magari kadhaa yalianguka katika maji baridi mapema Jumanne, na waokoaji wanawatafuta manusura wa ajali hiyo.
Waendeshaji wa mali hiyo ya mizigo walipoteza nishati ya umeme na kutoa tahadhari kabla ya chombo hicho kugonga katika daraja la Francis Key Scott, na kuiwezesha mamlaka ya usafiri kudhibiti idadi ya magari yaliyokuwa yanapita wakati huo katika daraja, Moore alisema.
Watu wawili waliokolewa, na haikuwa bayana wengine wangapi inawezekana wako ndani ya maji.
Chanzo cha habari hii ni kituo cha televisheni cha WJLA