Wakaazi wa Kyiv washtushwa na kughadhibishwa baada ya shambulizi

Athari za shambulizi la kombora lililopigwa na Russia karibu na Kyiv.

Jeshi la anga limesema wanajeshi wake wa ulinzi walitungua makombora yote yaliyorushwa baada ya kusitishwa kwa siku 44 katika mashambulizi hayo kwenye mji mkuu wa Ukraine. uharibifu huo umeonekana kusababishwa na vifusi vilivyoanguka.

Maafisa wa mji na mkoa wamesema takriban watu 13 wamejeruhiwa katika maeneo mbalimbali ya Kriv na wanne zaidi katika eneo hilo. msichana mwenye umri wa miaka 11 alikuwa miongoni mwa watu wanne waliopelekwa hospitali , maafisa wa mji wamesema.

Jeshi la Russia limetumia mabomu ya kimkakati na pia kurusha baadhi ya makombora kutoka katika eneo lake , makombora hayo yalilenga Kyiv kutoka pande tofauti , maafisa wa jeshi wamesema.