Jeshi linasema ndege kadhaa zisizo na rubani za Russia, zilitunguliwa mjini Odesa wakati wa shambulio la anga la usiku.
Shambulizi hilo limetokea wakati viongozi wa nchi za Magharibi walipokuwa wakijiandaa kukusanyika katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Jumamosi kuadhimisha mwaka wa pili wa uvamizi wa Russia, nchini Ukraine.
Viongozi hao akiwemo rais wa tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, walisafiri usiku kucha kwenda Kyiv, kwa treni.
Ukraine inawataka washirika wake wa nchi za Magharibi kuendelea kutoa misaada ya kijeshi ili ijilinde.
Forum