Viongozi wa Afrika watembelea Ukraine kwa juhudi za kumaliza vita vya Rashia na Ukriane

  • Abdushakur Aboud

Rais Vladimir Putin akutana na ujumbe wa viongozi wa nchi za Afrika mjini Saint Petersburg

Rais Vladimir Putin  akutana na viongoiz wa nchi za Afrika mjini Saint Petersburg

Rais Vladimir Putin (L) wa Rashia  na Rais Cyril Ramaphosa (R) wa Afrika Kusini wakutana kwenye Kasri Constantine (Konstantinovsky) kabla ya mkutano na ujumbe wa viongozi wa Afrika.

Rais Volodymyr Zelensky akutana na ujumbe wa viongozi wa nchi za Afrika mjini Kyiv.

Marais Ramaphosa, wa Afrika Kusini, Sall, wa Afrika Kusini, Hichilema, wa Zambia, Assoumani wa Comoros na waziri mkuu wa Misri Madbuly watoka ikulu ya Kyive baada ya kukutana na rais Zelensky wa Ukraine.

Rais Zelensky wa Ukraine (kushoto), akihudhuria mkutano na waandishi habari pamoja na viongozi wa nchi za Afrika baada ya mkutano wao mjini Kyiv.

Ujumbe wa amani wa viongozi wa nchi za Afrika watoa heshima zao mbele ya kaburi walozikwa watu wengi mjini Bucha.

Ujumbe wa viongozi wa Afrika watembelea maonesho ya picha ya watu walouliwa mjini Bucha.

Mwendesha mashtaka wa Ukraine Andriy Kostin  awaeleza viongozi wa nchi za Afrika kuhusu kilichotokea mjini Busha mnamo siku za mwanzo za uvamizi wa Rashia Ukraine.

Ujumbe wea viongozi wa Afrika watembela kaburi walozika watu wengi mjini Bucha, Ukraine na kuweka mshuma kutoa heshima zao kwa watu walouliwa kikatili huko.

Viongozi wa Afrika wakishauriana ndani ya treni wakielekea Kyiv, Ukraine kutoka Warsaw Poland kwa lengo la kutafuta njia za kuitisha mkutano wa amani kati ya Ukraine na Rashia 

Marais Macky Sall wa Senegal, Hakainde Hichilema wa Zambia Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini na Assoumani Azali wa Comoros,watembelea Ukraine kujaribu kutafuta njia za kuwaleta marais Volodomyr Zelensky wa Ukraine na Vladimir Putin wa Rashia kwenye meza ya mazungumzo.