Mgodi wa kobalti DRC wahitaji suluhisho la pamoja

Wachimbaji wadogo wadogo wakiwa katika mgodi wa madini ulioko jirani na mji wa Numbi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 7 Aprili 2017. Picha na Griff Tapper / AFP.

Matatizo yanayokabili uchimbaji wa madini ya kobalti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yanahitaji "muungano wa pamoja ili kuyatatua," kulingana na kampuni ya Microsoft.

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Marekani yenye thamani ya dola trilioni 1.9 hivi karibuni ilikuwa nchini DRC kujionea hali ya mfumo wa usambazaji wa vifaa vya elektroniki unavyoonekana.

Mkuu wa wafanyakazi, teknolojia na uwajibikaji katika kampuni ya Microsoft, Michele Burlington mwezi Desemba aliutembelea mgodi wa Mutoshi wenye wachimbaji wadogo wadogo wapatao 15,000, wakiwemo watoto wanaofanya kazi katika mazingira hatari sana.

Cha ajabu ni kwamba machimbo ya Mutoshi yalikuwa mgodi wenye mafanikio makubwa katika mfumo wa majaribio ili kurasmisha wachimbaji wadogo wadogo mpaka pale ulipofungwa mwaka 2020 kutokana na masharti ya virusi vya corona.

Nchi za Magharibi bado zinahitaji kobalti kutoka Kongo na kila mtu anakubali kwamba urasimishaji ndio suluhisho kwa binadamu na gharama za kiuchumi za uchimbaji wa madini.

Ripoti ya Biashara na Haki za Binadamu, kuhusu hali ya sasa ya mgodi wa Mutoshi, inaelezea ongezeko la wachimbaji wadogo wadogo kutoka 5,000 chini ya mpango wa mradi wa urasimishaji kwa kipindi cha miaka miwili hadi kufikia 15,000, pamoja na kuendelea kutojumuisha wafanyakazi wanawake, kurejea kwa ajira kwa wafanyakazi watoto na kushuka haraka kwa hali ya usalama wakati uchimbaji ukiondoka kwenye ule wa wazi na kurejea kwenye uchimbaji wa kienyeji.

Chanzo cha taarifa hii ni Shirika la habari la Reuters