Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:46

Sarafu ya DRC imeshuka thamani kutokana na mapigano


Sarafu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). July 3, 2012.
Sarafu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). July 3, 2012.

Kulingana na takwimu rasmi na wabadilishaji fedha ni kwamba sarafu ya Kongo imepungua thamani kwa takriban asilimia 15 dhidi ya dola ya Marekani jambo lililopelekea kuwaathiri watu walio maskini zaidi

Kuporomoka kwa sarafu ya ndani, malipo ya malimbikizo ya mishahara na matumizi ya vita yamepandisha bei za bidhaa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuwaacha wenyeji wakihangaika kumudu mambo ya msingi.

Tangu mwaka mpya wa 2023 sarafu ya Kongo imepungua thamani kwa takriban asilimia 15 dhidi ya dola ya Marekani kulingana na takwimu rasmi na wabadilishaji fedha na hivyo kuwaathiri watu walio maskini zaidi.

Watu kadhaa waliohojiwa na shirika la habari la AFP walisema katika baadhi ya bidhaa ni kwamba bei iliongezeka mara mbili au zaidi ya hapo. Ongezeko la bei linafuatia serikali kuongeza matumizi katika mapambano yake na kundi la waasi la M23 ambalo limeteka eneo kubwa huko mashariki mwa Congo tangu mwaka jana.

XS
SM
MD
LG