Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 07:11

Boti yapinduka ziwani na kuua watu sita DRC


Boti zinaandaliwa kusafirisha magunia ya mchele kutoka jimbo la Tshopo kwenda maeneo jirani ya jimbo hilo la DRC tarehe 31 Agosti 2022. Picha na Guerchom Ndebo/AFP.
Boti zinaandaliwa kusafirisha magunia ya mchele kutoka jimbo la Tshopo kwenda maeneo jirani ya jimbo hilo la DRC tarehe 31 Agosti 2022. Picha na Guerchom Ndebo/AFP.

Takriban watu sita wamefariki dunia na wengine darzeni hawajulikani walipo, baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kupinduka kutokana na upepo mkali kwenye Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mamlaka ya eneo hilo ilisema Jumatatu.

Boti hiyo ilikuwa imebeba wafanyabiashara na bidhaa zao wakitoka eneo la Mugote huko jimbo la Kivu Kusini na kwenda Goma mji mkuu wa jimbo jirani la Kivu Kaskazini.

Afisa wa polisi wa eneo la Mugote alisema upepo mkali ulisababisha mashua hiyo kuzama umbali wa kilomita 20 baada ya kuanza safari.

Afisa mwingine wa eneo hilo, kutoka Kivu Kusini, alisema mashua hiyo ilikuwa imebeba takriban abiria 150, 80 kati yao waliweza kujiokoa.

Alisema miili ya wanawake watatu na watoto watatu imepatikana wakati zoezi la kuwatafuta waathrika likiendelea.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina barabara chache zinazopitika, hivyo usafiri wa kwenye maziwa na mito ni muhimu kwa kuyafikia maeneo mengi . Hata hivyo, ajali za meli zimekuwa ni jambo la kawaida nchini humo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG