Mapigano hayo katika mji wa Soledar yamesababisha hasara kubwa kwa pande zote.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, katika hotuba yake usiku kila siku Jumatatu, aliuelezea uharibifu wa Soledar akisema “hakuna kuta zozote zilizobakshwa.”
“Kutokana na ukakamavu wa wapiganaji wetu huko, Soledar, tumeweza kupata muda wa ziada na nguvu ya ziada kwa Ukraine,” Zelenskyy alisema.
Takriban kilomita 10 kutoka Soledar ni mji wa Bakhmut, ambao wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema katika tathmini yake ya hivi karibuni ya kila siku inawezekana lengo kuu la Russia ni kuiteka Ukraine.
“Licha ya kuongezeka shinikizo kwa Bakhmut, Russia haielekei itaukamata mji huo kwa haraka kwa sababu majeshi ya Ukraine yanaendelea kushikilia eneo kubwa la kujihami na kudhibiti njia za kusafirisha mahitaji muhimu,” Wizara ya Uingereza ilisema.
Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani, aliyezungumza na waandishi Jumatatu kwa sharti jina lake lisitajwe, ameyaita mapigano huko Bakhmut “ ni ya kinyama.” kabisa.
Baadhi ya taarifa katika repoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya Some AP Reuters and AFP.